KilimanjaroPlanetarium

Juhudi zaidi zinahitajika kuvutia watoto masomo ya sayansi

Juhudi zaidi zinahitajika kuvutia watoto masomo ya sayansi

KATIKA kuhakikisha kuwa wanafunzi wengi zaidi wanalipenda somo la sayansi, Taasisi ya Longitude Technologies imeanzisha program iitwayo ‘STEM Club’.

Program hiyo ambayo ni mpya nchini Tanzania, wameanzisha kama utafiti wa majaribio katika Shule ya St. Rosalia ya jijini Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa progamu hiyo juzi, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi huyo, Musa Mishamo alisema lengo la kuanzisha program hiyo ni kuwavutia wanafunzi kuingia katika mambo ya sayansi na teknolojia kwa kufanya majaribio mbalimbali.

Alisema katika Shule ya St. Rosalia wanafunzi zaidi ya 400 watanufaika na program hiyo ya majaribio ambayo tayari imeonesha kufanya vizuri nchini Kenya kwa shule zaidi ya 1,000.

“Tunatumia vifaa mbalimbali ikiwemo Telescope kwaajili ya kuangalia anga moja moja, tunaangalia mwezi sayari, nyota na jua na vitu mbalimbali vinavyoendelea katika anga. Pia kifaa kingine ni sehemu ambayo watu wanaweza kuingia na kujifunza mbalimbali ya teknolojia na tunafundisha wanafunzi program ya kuttrack magari, pikipiki na kuongeza usalama katika jamii.

“Lengo ni kuwafanya wanafunzi kwenda katika ulimwengu wa teknolojia kwa kuwaonyesha ambazo ziko nje ya nchi. Kwa Tanzania ni mara ya kwanza na tunaifanya kama somo la majaribio na badaye itasambazwa katika shule mbalimbali mijini na vijijini,” alisema Mishamo.

Juhudi zaidi zinahitajika kuvutia watoto masomo ya sayansi

Mwalimu Mkuu Msaidizi wa St Rosalia, Oscar Kondowe alisema wamefurahishwa na ujio wa program hiyo katika shule yao wanaamini itawasaidia wanafunzi wao katika masomo ya sayansi na kujifunza teknolojia.

“Tunajivunia kwa shule yetu kuwa ni shule ya kwanza kufanya majaribio ya program hii nchini, sisi walimu tutajitahidi maarifa tuliyoyapata hapa tuweze kuwaelekeza na wanafunzi wetu. Nimejifunza vitu vingi kama mwalimu wa sayansi hivyo naweza kuwaelekeza na watu wengine,” alisema Kondowe.

Mwanafunzi wa darasa la saba katika shule hiyo, Leonard Daud alisema kuna faida katika kujifunza kwa vitendo kwani inasaidia kukumbuka kwa urahisi.

“Tunajiandaa na mitihani, kwa hiyo tunaposoma vitu kwa vitendo hata tunapokuwa tunajibu mitihani tunakuwa na uelewa zaidi na kuweza kufaulu mitihani yatu,” alisema Daud.

 Augustina Florence,  mwanafunzi wa darasa la saba katika shule hiyo alisema amefurahi ni mara ya kwanza kuona Telescope, kwasababu shuleni wanaoneshwaga kwenye vitabu.

“Ninapenda sana masomo ya sayansi, na ndoto yangu ni kuja kuwa  daktari ili niweze kuhudumia watu mbalimbali wenye matatizo ya kiafya, nafurahi sana nikimuona mtu ni mzima, kwahiyo mafunzo haya yananihamasisha zaidi ili niweze kufikia ndoto yang,” alisema.

Published by GETRUDE MBAGO at NIPASHE

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Scroll to Top